Wednesday, 24 April 2019

Usafi ni wajibu wa kila mtu.



MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge amefanya ziara katika Wilaya ya Kongwa,yenye lengo la kukagua maendeleo ya utoaji wa vitambulisho vya wajasiliamali ambapo,amekutana na changamoto ya baadhi ya wajasiliamali kugoma kufanya usafi kutokana na wao kuwa wamelipia kitambulisho.

Akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya hiyo Deo Ndejembi,Dkt Mahenge amefika na kuzungumza na baadhi ya wajasiliamali wanaofanya biashara zao katika eneo la mji mdogo wa Kibaigwa,ambapo Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa minadani na magulioni wilaya ya Kongwa Charles Magimba,amesema baadhi ya wafanyabiashara waliopo minadani suala la usafi kwao limekuwa ni shida kufanyika kutokana na madai kuwa wamekwisha lipia vitambulisho.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Deo Ndejembi ,amesema kuwa ni kweli walitoa maelekezo kuwa watu wasichangishwe gharama yoyote lakini kama wamejipangia uataratibu wao ni sawa.


Akitolea ufafanuzi suala hilo Mkuuwa Mkoa wa Dodoma Dkt.Mahenge yeye amesema kuwa usafi ni wajibu wa kila mtu na kama wao wamekubaliana wenyewe kuchangishana suala hilo halina tatizo.

Katika zoezi hilo wajasiliamali hao wamekiri kuwa vitambulisho hivyo vimekuwa na msaada mkubwa katika uendeshaji wa biashara zao kwani kwa sasa hawabugudhiwi kama hapo awali

0 comments:

Post a Comment