Wednesday, 24 April 2019

Serikali kuja na mkakati mpya.



Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inatarajia kuweka mkakati wa pamoja wa kuanza programu ya mabadilishano ya shughuli za kujitolea nchini ambazo zitaweza kubainisha utaratibu wa kupokea vijana wa kujitolea kutoka nje ya nchi.
Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Mkurugenzi msaidizi uratibu na uwezeshaji vijana kiuchumi kutoka ofisi ya waziri mkuu Esther Riwa wakati akifungua mkutano wa Raleigh Tanzania iliyolenga kuelezea mafanikio ya shirika hilo kwa vijana.
Amesema kupitia utaratibu huo wa kuanzisha programu ya kujitolea utawezesha kuwafikia vijana wengi zaidi kupata ujuzi, kubadilishana maarifa ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inatarajia kuweka mifumo mizuri ambayo itawezesha vijana kupata taarifa za masuala mbalimbali yanayoendelea ili waweze kuzitumia kwa ajili ya maendeleo yao.
Amesema zipo kazi nyingi zilizofanyika lakini taarifa hizo haiwanufaishi vijana kutokana na kukosekana kwa mifumo mizuri ya upatikanaji wake.
Kwa upande wake Ofisa wa mradi wa uwajibikaji wa jamii kupitia vijana Peter Lazaro amesema lengo la mradi huo ni kutoa elimu kwa vijana ili wawajibike, ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amesema wanafuatilia maendeleo ya miradi iliyokamilika na inayoendelea katika maeneo mbalimbali wanaishi vijana ili kuifanya miradi hiyo kuwa endelevu na kuleta tija kwa jamii.

Aidha vijana hao wamesisitizwa suala la uanzishwaji wa vikundi vya vijana vyenye muelekeo wa uchumi wa kati wa viwanda

0 comments:

Post a Comment