Baraza la
wafanyakazi wa wizara ya fedha na mipango limetakiwa kufuatilia risimali fedha
zinazotolewa kama zinatumika ipasavyo na kusimamia utekelezaji wa bajeti
zinazotolewa na serikali kuhakikisha zinawafikia wananchi wakawaida lengo likiwa nikujenga
uchumi wa viwanda na kuchochea mageuzi ya uchumi na maendeleoa ya watu.
Hayo
yamesemwa na naibu waziri wizara ya fedha na mipango dr.ashatu kijaji (mb)
wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara ya fedha na mipango
jijini Dodoma.
“”tunahitaji
kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuziya uchumi wetu,maendeleo yetu
sisi wanyewe pamoja na wananchi,hususani maendeleo ya watu wa kipato cha
chini””
Aidha ashatu
kijaji amelitaka baraza hilo kufanya kazi kwa ushirikiano,umoja,mshikamano,ufanisi
na uadilifu pamoja na kuzingatia kanuni,sheria,taratibu na miongozo iliyopo
katika wizara hiyo.
“napenda kuchukua nafasi hii kusisitiza
umuhimu wa kufanya kazi zetu kwa ushirikiano,umoja,mshikamano na
ufanisi,tuzingatie sheria ,kanuni na utaratibu wa miongozo””
Kwa upande
wake mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi wa wizara ya fedha na mipango doto
james amesema kuwa baraza hilo limeleta mafanikio mbalimbali ikiwemo kuboresha
huduma kwa watumishi,kuboreshwa kwa mazingira ya kufanyia kazi ikiwemo
kuwapatia watumishi vitendea kazi.
“”miongoni
mwa mafanikio yaliyotokana na baraza la wafanyakazi la wizara yetu ni kuboresha
huduma kwa watumishi na mazingira ya kufanyia kazi kwa kuwapatia watumishi
vitendea kazi””
Nae naibu
katibu mkuu wizara ya fedha na mipango dr.khatibu kazungu ameahidi
kushughulikia suala la utoaji huduma bora kwa wafanyakazi hususani wasitafu
ambao wanahitaji mafao yao ya usitafu.







0 comments:
Post a Comment