Wednesday, 17 April 2019

Maagizo ya mkuu wa mkoa wa Dodoma ,baada ya kuwasili chemba.


MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dk.Binilith Mahenge  ameonyesha kusikitishwa na maendeleo ya ujenzi wa hospital ya wilaya ya Chemba na hivyo kuagiza hadi kufikia mwezi May mwaka huu ujenzi huo kuwa umekwisha kamilika.

Dk.Mahenge ametoa maagizo hayo hii leomara baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzin wa Hospital hiyo ambapo ameitaka Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanaondoa  vikwazo vyote vinavyopelekea ucheleweshaji wa ujenzi huo ikiwa ni pamoja na kuongeza mafundi ili kazi iende kwa uharaka zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Saimon Odunga amesema atakaa na kuzungumza na mafundi hao ili kujua changmoto inayowakwamisha ambapo hata hivyo watalazimika kuongeza mafundi ili kuhakikisha kazi hiyo inakwenda kwa haraka zaidi.

Wakizungumzia madai ya mafundi kutolipwa fedha zao Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Dr.Semistatus Mashimba na kaimu mhandisi wa wilaya hiyo Filomena Bango wao wamekanusha madai hayo na kusema kuwa mafundi wote wakwishalipwa fedha zao katika awamu ya kwanza ya ujenzi ambayo imekwishakamilika.

Hata hiyo mara baada ya baadhi ya mafundi kuhojiwa juu ya madai ya kutolipwa fedha zao mafundi hao wamekana na kusema kuwa wamekuwa wakilipwa fedha zao kwa wakati na hadi sasa wanaendelea na kazi vizuri

0 comments:

Post a Comment