Monday, 15 April 2019

Mkakati mpya wa kimazingira mkoani dodoma Waja.


Mkoa wa Dodoma umepanga mikakati kwa kila mtu kufanya usafi katika makazi yake na mita 5 kuzunguka nyumba yake pamoja na taasisi zote katika mkoa huo lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya mkoa huo na kuendelea kushika nafasi bora za usafi kitaifa.

Hayo yamesemwa na afisa afya wa mkoa huo Kali Sailas Lyimo katika mkutano uliofanyika wa wadau wa usafi wa vyoo na mazingira mkoani humo wa kujadili mikakati ya uboreshaji wa mazingira wa mkoa huo.

Kwa upande wake mratibu wa kampeni ya usafi wa mazingira mkoa wa Dodoma francis muliku amesema kuwa mkoa wa Dodoma umekuwa na mafanikio makubwa sana ya usafi wa mazingira ambapo idadi ya kaya zenye  vyoo bora imeongezeka katika mkoa huo.

Nae mratibu wa afya shule za jiji la dodom mwalimu theresia mudaha ameelezea changamoto za vyoo zilizopo katika jiji hilo na kusema kuwa usafi wa mazingira shuleni ni mzuri katika jiji hilo.

Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya chamwino Kathibeti kongola amesema kuwa katika halmashauri hiyo ya chamwino idadi ya nyumba zenye vyoo imepanda kutoka asilimia 81% hadi asilimia 99.62 katika halmashauri hiyo.



0 comments:

Post a Comment