Yanga waibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC
Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao KMC katika mchezo uliochezwa Leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam licha ya kufungwa mapema dakika ya 16.
Mpaka mapumziko timu zote zilikuwa zimetoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 hali iliyowafanya KMC waamini kwamba watarejea na pointi moja kutoka kwa vinara wa ligi kwa sasa Yanga ambao wana pointi 70.
KMC waliongeza moto wa mashambulizi kipindi cha pili ambapo kocha wa KMC Ettiene Ndirayagije alianza kwa mabadiliko kwa kumtoa mlinda mlango Jonathan Nahimana nafasi yake ikachukuliwa na Juma Kaseja.
Dakika ya 62 Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alifanya mabadiliko ya kiufundi kwa kumtoa Deus Kaseka akaingia Ibrahim Ajibu na Thaban Kamusoko nafasi yake ikachukuliwa na Amiss Tambwe.
Mabadiliko hayo yalileta matokokeo chanya kwani dakika ya 67 Ibrahim Ajibu alipiga pasi moja kumtamfuta Tambwe iliyomaliziwa na beki wa KMC Ally Ally ambaye alijifunga kwa kichwa safi kilichomshinda Kaseja wakati akiokoa mpira.







0 comments:
Post a Comment