Jack Grealish ashambuliwa na shabiki Uwanjani
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Aston Villa Jack Grealish ameshambuliwa na shabiki aliyekimbilia uwanjani katika mechi ya Aston Villa dhidi ya mahasimu wao Birmingham Villa Jumapili.
Shambulio hilo lilitokea katika takika ya 10 wakati mwanamume aliyekuwa amevalia kofia alipojitosa uwanjani na kupita nyuma yake kabla ya kupitisha mkono wake hadi kwenye uso wa Grealish.
Shabiki huyo ambaye alikuwa amevalia jaketi ya Birmingham City, alibusu mikono yake huku akiashiria kutuma busu zake kwa umati wa mashabiki alipokua akiondoshwa Uwanjani.
Polisi wa kituo cha West midlands wamesema mwanamume huyo amekamatwa kufuatia tukio hilo, Wageni walishinda mchezo huo kwa 1-0, huku Grealish akipata bao la ushindi mnamo dakika ya 67 ya mchezo







0 comments:
Post a Comment