Monday, 11 March 2019

Watu 23 wafariki kufuatia amvua kali zilizonyesha

Watu 23 wafariki kufuatia amvua kali zilizonyesha

Mvua kali zilizonyesha nchini Malawi zasababisha vifo vya watu 23. Mvua ambazo zilizambatana na upepo zimenyesha nchini Malawi na kusababisha maafa hayo.

Waziri wa afya wa Malawi Nicholas Dausi  amewafahamisha waandishi wa habari kuwa mvua kali zilizonyesha kwa muda wa siku nne mfululizo Kusini mwa Malawi  zimepelekea watu 23 kufariki.

Majumba zaidi ya 20 000  yamebomolewa na mvua ahizo ambapo pia watu zaidi ya 100 wameripotiwa kujeruhiwa.

Waziri wa afya katika tanagazo alilotoa Jumamosi amefahamisha kuwa watu 11  hawajulikani walipo baada ya mvua hizo kunyesha.

0 comments:

Post a Comment