Wasanii waguswa na kifo cha Mtangazaji Ephraim Kibonde
Mapema asubuhi ya leo tasnia ya habari nchini imepata pigo kufuatia kifo cha Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Ephraim Kibonde.
Watu mbalimbali wametuma salamu za pole kufuatia kifo cha mtangazaji huyo maarufu nchini, wasanii nchini pia wameonyesha kuguswa na kifo chake. Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, chini ni kile walichoandika;
Elizabeth Michael LULU: Katika Kila FURAHA Na HUZUNI,Katika Kila TAABU Na MATESO,Katika Kila MEMA Na MABAYA.....Wewe Ni MUNGU na Utabaki Kuwa MUNGU....Hatuwezi Kusema ZAIDI....Hatuwezi Kusema PUNGUFU.
Mimi Mars: Dah Poleni sana familia yangu ya Clouds Media pamoja na familia ya
Ephraim Kibonde Mwenyezi Mungu awape nguvu katika kipindi hiki Poleni sana Rest Easy Ephraim Kibonde.
Stamina: Daaah poleni sana ndugu,jamaa,familia na marafiki wa kaka yetu KIBONDE,pole sana sana sana uongozi mzima wa CLOUDS...kipindi kigumu hichi ila kitapita tu...tuombe Mungu.
Katarina Karatu: Tuseme nini sasa Mungu wetu wewe umeamua kumchukua aliye wako tunaumia sana lakini MUNGU ANABAKI KUWA MUNGU.... wale watoto Mungu tunakuomba uwape faraja itokayo kwako sisi kwa akili zetu hatuwezi Mungu wetu R.I.P kaka Kibondeππππ.
AY: Nimestushwa sana na taarifa ya kifo chako Kaka yangu...Pumzika kwa Amani Kaka Yangu #EphraimKibonde...Tumeshirikiana kwenye Mengi ya Kikazi na Familia..Pumzika kwa Amani Wakukaja ππΏππΏππΏππΏ Tusali sana ha-tujui Siku wala Saa
/...Mbele ni giza ila Sala ndio Taa
Lady Jaydee: Hili ni jambo zito kwa watu wenye ukaribu na Ephraim Kibonde.
Tunakaa tunakunywa, tunacheka siku nyingine mmoja wetu anatwaliwa π
Mwenyezi Mungu wa rehema ukawafariji watoto, ndugu, jamaa na marafiki kwa pigo hili.
Tunashukuru kwa kila jambo .
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amethibitisha kwamba Mtangazaji huyo amefariki akiwa Mwanza, alianza kusumbuliwa na Presha toka Bukoba kwenye msiba wa Ruge Mutahaba na kuhamishiwa Mwanza. Kifo cha mtangazaji huyo kinakuja siku chache baada kufariki Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media,Ruge Mutahaba.








0 comments:
Post a Comment