Thursday, 7 March 2019

DUP na matokeo bora ya sekta ya Afya Nchini

DUP na matokeo bora ya sekta ya Afya Nchini



Serikali yaTanzania imejiwekea mkakati wa Kitaifa wa kuboresha matumizi ya takwimu za afya, utakaosaidia kuboresha utoaji wa huduma katika Sekta ya Afya, ambao unaitwa 'Data Use Partnership' DUP

 Mpango huu unalenga kujenga utamaduni wa ukusanyaji na matumizi ya takwimu katika sekta ya afya.

 Uwepo wa Mifumo mingi iliyopo katika sekta ya afya unapelekea mifumo hiyo kushindwa kuwasiliana (visiwa vya taarifa). Mpango huu umeanzishwa ili kuboresha mfumo mzima wa taarifa na takwimu, hali itakayosaidia kuimarisha utoaji huduma katika Sekta ya Afya.

 Mpango wa kuboresha matumizi ya takwimu utasaidia kutatua changamoto mbalimbali katika Sekta ya Afya mfano Magonjwa ya Mlipuko, kutambua vituo vyenye utendaji unaoridhisha na usioridhisha

Mpango wa kuboresha matumizi ya takwimu za afya Tanzania hauishii kuhamasisha mfumo wa Afya wa kidijitali tu, pia Unajenga uwezo wa kutumia takwimu hizo.

Sekta ya afya lazima iingize utamaduni wa matumizi ya taarifa ili kuimarisha utawala na sera.
Matumizi sahihi na ya mara kwa mara ya takwimu yatapelekea maamuzi sahihi, mifumo kuboreshwa na matokeo mazuri katika sekta

Takwimu sahihi zinazopatikana kwa wakati zinawawezesha wahudumu wa afya kufanya maamuzi sahihi pale wanapotoa huduma za Afya katika vituo vyao.

 Mpango wa kuboresha matumizi ya takwimu za afya unafanya kazi kuakikisha kila mmoja kuanzia watumishi wa serikali, wahudumu na wateja wa afya wanaweza kufanya maamuzi sahihi ya afya.

0 comments:

Post a Comment