Wakili huyu atangaza kugombea nafasi ya Urais TLS
Wakili wa Kujitegemea Godfrey Wasonga ametangaza kugombea nafasi ya Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amesema kuwa endapo atachaguliwa atafanya ushawishi wa kubadilisha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma amesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa rais wa TLS mojawapo ya jambo ambalo atalipigania ni kuhakikisha anatumia nafasi yake kufanya ushawishi wa kubadilisha katiba ya Tanzania ili kuondoa sheria kandamizi.
"Kwa sasa hakuna demokrasi ya kweli kutokana na kuwepo kwa katiba iliyopitwa na wakati ambayo haiendani na matakwa ya kidunia ya sasa"amesema Wasonga.
Aidha Wakili Wasonga amesema kuwa ikumbukwe kuwa katiba tuliyonayo kwa sasa niyamwaka 1964 ,ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 1977 hivyo kwa sasa haiwezi kuendana na matakwa ya kidunia
Wakili huyo amesema kuwa kama hakuna katiba yenye kurekebishwa na kuondoa sheria kandamizi nchi haiwezi kuwa na demokrasia ya kweli na ikiwepo katiba nzuri itaweza kumsaidia hata rais aliyepo madarakani.
Hata hivyo Wasonga amesema kuwa iwapo atapata nafasi ya kuwa rais atakuwa na vipaumbele vitano ambavyo ni kubadilisha katiba ya TLS kutoka kufanya uchaguzi kwa mwaka mmoja na kuwa miaka miwili.
"Endapo nitachaguliwa pia nitaboresha huduma kwa wanachama hasa katika bima ya Afya ili kila wakili awe na bima ya afya ambayo itaweza kumsaidia yeye na familia yake"alisisitiza
"Pia nitakiondoa kipengele cha ulipaji wa ada ambayo hulipwa kila mwisho wa mwaka na badala yake iwe inalipwa mwanzo wa mwaka au wakati wowote na siyo lazima mwisho wa mwaka" amesema Wasonga.
Wakili Wasonga amesema kuwa katika uongozi wake atakuwa na sera ya pensheni kwa mawakili ambao watakuwa wamefikia uzeeni ili wawe na kitu ambacho kitaweza kuwasaidia.
"Ada za mawakili zimekuwa zikiongezeka kutoka sh.30000 hadi kufikia sh.50000 , na ili uweze kufika katika vikao vya mawakili ni lazima ulipe kiasi cha sh.120,000 lakini katika uongozi wangu nitaishusha hadi kufikia kiasi cha sh. 60000 kama ilivyokuwa awali ili kumpunguzia mwanachama badala ya kumuongezea gharama.
Hata hivyo Wasonga amesema kuwa katika uongozi wake atatoa elimu juu ya ujasiriamali ambao utaweza kumsaidi wakili pale ambapo hatakuwa na kazi.







0 comments:
Post a Comment