Jumla ya Vijana 6 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya Bangi,Mirungi na kokeini.
Vijana hao ni Khamis Hamadi Salum,Ali Hemedi Ali, Ali Moh’d Ahmada,Ali Rajab Hassan, Sofia Abdallah Mbarouk na Juma Mbarouk Said.
Akithibitisha kukamatwa kwa vijana hao Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Thobias Sedoyeka alisema kati ya kipindi cha wiki moja kuanzia tarehe mbili hadi kumi na moja jeshi la Polisi limefanikiwa kuwatia nguvuni vijana 6 kati yao Mwanamke Mmoja kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya Bangi na Kokein.
Alisema vijana hao hao walikutwa katika maeneo tofauti tofauti ndani ya mkoa huo ambapo wote bado wanashikiliwa naJeshi la Polisi kwa hatua za kisheria.
Kamanda alifafanua kuwa Mnamo Tarehe 02 March mwaka huu kijana Khamisi Hamadi Salum miaka 37 kabila Mshirazi, Mkaazi wa Mtoni alikamatwa akiwa na Mirungi.
"Kijna mwingine ni alikamatwa tarehe 3 mwezi huu maeneo ya fuoni Ali Hemedi Ali miaka 29 akiwa na nyongo 26 za bangi na mwingine ni alikamatwa tarehe 6 pia mwezi huu maeneo ya Daraja bovu ni ALI Mo’hd Ahmada miaka 18 akiwa na nyongo 13 na furushi moja la Bangi," alifanua Kamanda.
Aidha aliwataja wengine ni walikamatwa tarehe 4, 25 na tarehe 7 ambapo alikamatwa maeneo ya Raha leo,Chuini na Mwanakwerekwe wakiwa na Bngi nyongo 213, dawa za kulenya aina ya vijiwe vitano vya dawa za kulevya na mwingine vijiwe 25 za dawa hizo za kulevya aina kokeini.
Katika hatua nyingine Kamanda huyo aliwaomba wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu







0 comments:
Post a Comment