Monday, 11 March 2019

Update: Kisanduku cheusi cha ndege ya Ethiopian Airlines chapatikana

Update: Kisanduku cheusi cha ndege ya Ethiopian Airlines chapatikana


Kisanduku cha kutunza kumbukumbu za ndege ‘Black Box’ cha ndege ya Ethiopian Airlines Boeing 737 kimepatikana.

Kifaa hicho ni muhimu kwenye uchunguzi wa kubaini kilichosababisha ajali ya ndege hiyo kwani ndicho chenye kunakili data zote muhimu.

Ndege ya Ethiopian Airlines Boeing 737 Max-8 alianguka mapema hapo jana ambapo Watu 149 walifariki pamoja na wahudumu 8. Ndege hii aina ya Boeing 737 Max-8 ni ya pili kuanguka katika kipindi cha miezi 5.

0 comments:

Post a Comment