Monday, 11 March 2019

Simba SC waondoka kwa Waarabu

Simba SC waondoka kwa Waarabu


Jioni ya leo Msafara wa timu ya Simba SC umeondoka nchini Algeria kurejea nyumbani
Tanzania kwa kupitia Dubai.

Simba SC walikuwa nchini humo kwa ajili ya mchezo wa raundi ya nne klabu bingwa Afrika
dhidi ya JS Saoura. Kikosi hicho kinarejea nchini tayari kujiandaa na mchezo dhidi ya AS Vita kutoka nchini DR Congo.
Hadi sasa Simba SC wanashika mkia kwenye kundi lao wakiwa na pointi sita pekee walizojikusanyia katika michezo mitano waliyocheza hadi sasa. Iwapo watashinda mchezo wao wa mwisho Simba SC watajihakikishia nafasi ya kucheza robo fainali.

0 comments:

Post a Comment