Mkoa wa Geita watekeleza agizo la Rais Magufuli
Agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli kujengwa kwa masoko ya madini kwenye Mikoa yenye rasilimali hiyo latekelezwa Geita.
Geita ni Mkoa ambao unaongoza kwa uzalishaji wa Dhahabu nchini kwa zaidi ya asilimia 40.
Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel leo amezungumza na waandishi wa habari ujio wa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Soko Kuu la Dhahabu Mjini Geita Machi 14 mwaka huu.
Kuanzishwa kwa soko la dhahabu kunatarajiwa kufungua fursa za kiuchumi kwa mkoa huo.







0 comments:
Post a Comment