Simba SC, Yanga SC zatozwa faini Mamilioni ya fedha na TFF
Klabu ya Yanga SC imetozwa faini ya Tsh. 6,000,000 (milioni sita) kwa kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi, kutoingia vyumbani na kusababisha wachezaji wakaguliwe kwenye korido, na pia kutotumia njia maalum iliyowekwa kwa ajili ya kuingia kwenye eneo la kuchezea (pitch).
Ni katika mechi hiyo iliyochezwa Februari 16, 2019 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Adhabu imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Wakati huo huo Simba SC imetozwa faini ya sh. 3,000,000 (milioni tatu) kwa kuingia uwanjani wakitumia mlango usio rasmi, lakini vilevile kutotumia njia maalum iliyowekwa kwa ajili ya kuingia kwenye eneo la kuchezea (pitch). Adhabu imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo
0 comments:
Post a Comment