Teknolojia inavyofanikisha huduma kwa mama mjamzito Tanzania
Kwa mara ya kwanza, teknolojia ya 'block chain' imefanikisha huduma kwa mama mjamzito kujifungua mtoto ambaye amesajiliwa chini ya mfumo huo katika mradi wa afya unaodhaminiwa na serikali ya Ireland.
Habari hii imeripotiwa na vyombo vya kimataifa, huku wataalam wa Afya wakieleza teknolojia hii inavyoweza kusaidia katika mtu kupata huduma za kiafya kwa urahisi na kwa ufanisi.
Block chain ikiwa ni huduma inayohusika na kutoa huduma zozote zile za kibiashara au kusaidia jamii kwa njia ya mtandao au kidijitali, ina uwezo wa kutunza kumbukumbu ya mfumo ya kifedha maarufu kama 'bitcoin na cryptocurrencies'.
Dr.Victor Kiyaruzi kutoka hospitali ya Kilema, Moshi anasema kwa upande wao wanatoa huduma hii ili kuwasaidia watu wenye matatizo ya afya kumfikia daktari kwa rahisi na unafuu.
"Teknolojia sasa hivi imekuwa na watu wengi wanatumia simu za mkononi 'smart phone' na hivyo mfumo huu unaweza kumsaidia mgonjwa kupata huduma ya afya.
GETTY IMAGES
"Mfano, watu wengi wamekuwa wakipata matatizo ya afya na kulazimika kusafiri kwa umbali mrefu kutoka eneo moja mpaka lingine na akifika hospitali anapanga foleni kwa muda mrefu kwa jambo ambalo angeweza kupata msaada kwa kumuuliza daktari kupitia mtandao", Daktari Kiyaruzi anaeleza.
Daktari Kiyaruzi aliongeza kusema kuwa mgonjwa anaweza kupata huduma ya ushauri kutoka kwa mtaalamu kupitia mtandao bila ya kufika hospitalini au mhudumu wa afya anaweza kumfuata alipo.
Teknolojia hii inayokuwa ya 'Blockchain' imelenga kuangaalia uwazi katika matumizi ya serikali, wadau wa maendeleo, mashirika yasiyo ya serikali na imeanzishwa kwa mfumo wa utambuzi wa kupatikana kwa huduma muhimu.

Mtoto alinufaikaje na Bitcoin
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Bitcoin Exchange Guide inasema kuwa teknolojia ya 'blockchain' inaweza kuweka taarifa kabla ya kujifungua, na kuwasaidia wanawake wajawazito wasiojiweza ili kusaidiwa kupata huduma muhimu kwa msaada wa kimfumo.
Kwa mara ya kwanza mwezi Julai mwaka jana, mtoto wa kwanza kwa kutumia teknolojia hii alizaliwa nchini Tanzania na kuongeza kwenye mfumo huu wa kidijitali.
Namna mfumo unavyofanya kazi
Kwa mujibu wa jarida la Forbes, mradi huu utampa kila mjamzito utambulisho maalum wa kidijitali ambao utawasaidia kuwapatia wajawazito Vitamin ikiwemo Folic acid, na kufuatilia maendeleo ya wanawake wajawazito kwa kutumia data zilizoongezwa kwenye mfumo wa blockchain.
Kuanzia usajili, msaada wa kimatibabu hadi kujifungua.
Mtoto wa kwanza kwa kutumia mfumo huu alizaliwa tarehe 13 mwezi Julai 2018 na kufuatia na wengine wawili walizaliwa tarehe 19 Julai 2018.







0 comments:
Post a Comment