Mshirika wa Trump ahukumiwa kifungo cha miezi 47 jela
Aliyekuwa mwenyekiti wa kampeni wa Rais wa Marekani Donald Trump, Paul Manafort, amehukumiwa kifungo cha miaka karibu minne gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kukwepa kulipa kodi na udanganyifu wa kibenki unaohusishwa na kazi yake ya kuwashauri wanasiasa wa Ukraine.
Manafort hakuzungumza chochote baada ya hukumu hiyo kutolewa dhidi yake.
Huku hukumu hiyo ikiwa ni kubwa kutolewa kwa mshirika wa Trump na tume maalum ya Robert Mueller, huenda ikawa mbaya zaidi kwa Manafort.
Tayari Manafort amekuwa gerezani tangu mwezi Juni, hivyo hukumu hiyo itaizingatia miezi tisa ambayo tayari amekaa gerezani.
Hata hivyo, bado anakabiliwa na uwezekano wa hukumu yake kuongezwa kutokana na kesi nyingine inayomkabili katika Mahakama ya District of Columbia.
chanzo DW.






0 comments:
Post a Comment