Friday, 8 March 2019

Kagame ana sababu ya kuizuru Tanzania, wasema wachambuzi.

Kagame ana sababu ya kuizuru Tanzania, wasema wachambuzi

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais Kagame aliishi Tanzania na kupata mafunzo ya kijeshi nchini humo
Ziara hii ya Bwana Kagame ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa Jumuia ya Afrika mashariki (EAC), ina umuhimu mkubwa sana kwake binafsi na pia kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla, amesema mchambuzi wamasuala ya siasa za kimataifa Mohammed Issa.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame yuko nchini  kwa ziara ya siku mbili kufuatia mwaliko wa mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli.
Ziara yake imekuja wakati uhusiano wake na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ukilegalega huku mpaka kati ya Rwanda na Uganda ukifungwa.
''Naweza kusema huenda amekuja kushauriana na mwenyeji wake Magufuli juu ya mzozo huu na labda kumtaka aingilie kati kujaribu kuupatia mzozo huu'' Aliieleza BBC Bwana Issa.
Kulingana na taarifa kutoka Wizara ya mambo ya nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, viongozi hao wanatarajiwa kujadili masuala mbali mbali kati ya nchi hizo mbili pamoja na ushirikiano wa kikanda.
Taarifa ya IkuluHaki miliki ya pichaIKULU TANZANIA
''Uhusiano baina Rwanda na Tanzania umeimarika zaidi wakati wa utawala wa rais wa sasa John Magufuli kinyume na ulivyokuwa enzi ya mtangulizi wake Jakaya mrisho Kikwete baada ya kuingia dosari, kikwete alipomtaka Bwana Kagame afanye mazungumzo na wanamgambo wa kundi la waasi FDLR lililopo mashariki mwa DRC ambao Rwanda inawatuhumu kutekeleza mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
'' Uhusiano wa sasa kati ya Magufuli na Kagame ni mzuri kwa kweli, ana kila sababu ya kuitembelea Tanzania wakati huu'' alisema Bwana Mohammed Issa.
Huenda wakajadili masuala ya kikanda
Marais Paul Kagame na mwenyeji wake John Magufuli wanategemewa kujadili suala tete la sheria mpya ya kibiashara iliyozua utata miongoni mwa wafanyabiashara wanaotumia malori, ambayo inapunguza uzito wa mizigo inayoisafirishwa kwenye barabara za Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki.
''Wafanyabiashara wa Afrika mashariki wameilalamikia sheria hiyo wakisema kuwa haitakuwa na tija kwa biashara zao, bila shaka viongozi hawa watajaribu kutafuta suluhu'' Ameileza BBC Bwana Mohammed Issa.
Wanatarajiwa pia kuzungumzia suala la mkataba wa kibiashara baina ya Muungano wa Ulaya na nchini wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kujaribu kupata msimamo mmoja wa kikanda kabla ya mazungumzo ya kusainiwa kwa mkataba huo.
Rwanda ambayo ni nchi isiyopakana na bahari huenda sasa ikaitegemea sana bandari ya Dar es salaam Tanzania zaidi kama kituo muhimu cha kupokea bidhaa zake zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, wakati huu ambapo uhusiano wake na Uganda umeingia dosari.
Rais wa kwanza wa Tanzania mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Image captionRais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius kambarage Nyerere alikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika wa kwanza walioizuru Rwanda baada ya mauaji ya 1994
Mamlaka mjini Kigali zimekuwa zikilalamikia matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu dhidi ya raia wake wanaoenda Uganda hata hivyo Uganda imekuwa ikikanusha tuhuma hizo.
Wiki hii Rwanda ilitangaza mpaka wake na Uganda wa Gatuna umefungwa kutokana na shughuli za ujenzi wa barabara unaoendelea, lakini wachanganuzi wa masuala ya kikanda walitaja hatua hiyo kama ulipizaji kisasi kwa Uganda kutokana na tumuma za uganyasaji wa wanyarwanda ndani ya Uganda.

Kagame ana historia na Tanzania

  • Rais Paul Kagame aliishi nchini Tanzania ambapo alipata mafunzo yake ya awali ya kijeshi katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Tanzania cha Monduli, kabla ya kurejea Uganda na hatimae kuanzisha vita vya ukombozi wa taifa lake miaka ya tisini.
  • Tanzania imekuwa na mchango mkubwa katika taaluma yake kama mwanajeshi.
  • Uhusiano wa Rwanda na Tanzania ulinoga zaidi baada ya vita na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, kutokana na hatua ya rais wa kwanza wa Tanzania julius Kambarage Nyerere kuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza wa kigeni kutangaza kuwa mauaji yaliyofanyika Rwanda mwaka 1994 yalikuwa ni ya kimbari.
  • Mwalimu Nyerere pia alikuwa miongoni wa viongozi wa kwanza wa kiafrika kufanya ziara nchini Rwanda baada ya mauaji hayo na kulihutubia bunge.
Rais wa Rwanda Paul Kagame na rais wa Tanzania Dokta john Pombe MagufuliHaki miliki ya pichaIKULU/VILLAGE URUGWIRO
Image captionRais wa Rwanda Paul Kagame akiwa pamoja na mwenyeji wake rais wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli
Rwanda kwa upande mwingine inanajivunia uhusiano mzuri wa kibiashara na Tanzania.
Mara ya mwisho rais Kagame alizuru Tanzania ilikuwa mwezi Januari mwaka 2018 kwa ziara rasmi.
Mwenzake rais Magufuli ambaye hapendelei sana kusafiri nje ya nchi alizuru Rwanda mwezi Aprili mwaka 2016.

0 comments:

Post a Comment