Kambi ya wazee hatarini kukumbwa na magonjwa
Wazee wanaolelewa kwenye kambi ya Busanda wilayani Shinyanga, wako hatarini kupatwa na mlipuko wa magonjwa kutokana na kujaa kwa choo wanachokitumia.
Choo hicho kilijengwa miaka mingi na sasa kimeshachoka na hakifai tena kwa matumizi, lakini kutokana na ukosefu wa choo, wazee hulazimika kukitumia hivyo hivyo.
Wazee walipaza kilio hicho jana, wakati maofisa wa maendeleo ya jamii ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, kwa kushirikiana na Shirika la PAWWCO linalojishughulisha na shughuli za kijamii mkoani hapa, walipotembea kuwapatia msaada wa nguo, chumvi na sabuni za kufulia.
Mmoja wa wazee hao, Elizabeth Mhari, alisema kambi hiyo imekuwa ikikabiliwa na ubovu wa choo kwa kuwa kilichopo ni kibovu na kimeshajaa na wamekuwa wakikitumia hivyo hivyo, hali ambayo imekuwa ikihatarisha usalama wa afya zao.
“Changamoto kubwa ambayo tunakabiliana nayo hapa ni ubovu wa choo kwa kuwa kimeshajaa kabisa. Tunaomba msaada wa kutengenezewa kingine hiki hakifai kabisa kinahatarisha usalama wa afya zetu,” alisema Mhari.







0 comments:
Post a Comment