Saturday, 9 March 2019

Giza nene latawala Venezuela

Giza nene latawala Venezuela

Umeme umekatwa katika maeneo mengi nchini Venezuela, hali  iliyosababisha mtafaruku nchini humo.

Kulingana na vyombo vya habari nchini Venezuela,umeme umekatika katika majimbo 22 kati ya majimbo 23 na hivyo kuiacha karibu nchi nzima bila umeme.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa hali kama hiyo haijatokea nchini Venezuela kwa miaka mingi.

Kukatika kwa umeme kumesababishwa na matatizo katika bwawa la Guri kusini mwa jimbo la Bolivar.

Bwawa la Guri ni kati ya mabwawa muhimu ya kusambaza umeme nchini Venezuela.

Hata hivyo waziri wa umeme Luis Motta Dominguez amesema kuwa hilo sio shambulizi dhidi ya serikali bali ni shambulizi dhidi ya wananchi.

0 comments:

Post a Comment