Kiongozi mkuu wa dini nchini Iran
amesema kuwa taifa hilo halitashirikiana na Marekani pamoja na Uingereza
kuhusu maswala kadhaa ya kieneo.
Katika hotuba iliopeperushwa runingani, Ayatollah Khamenei alisema kuwa malengo ya Marekani katika eneo la mashariki ya kati hayaingiliani na Iran.
Khamenei ameishtumu Marekani akisema licha ya kukubaliana na Iran kuhusu mpango wake wa nuklia kuwaamni ni makosa makubwa.
''Shetani Marekani na Uingereza walikuwa wakitumia unyanyasaji wa haki za kibinaadamu na zile za kigaidi ili kutoafikia makubaliano hayo''.
Bw Khameneo alikuwa akizungumza katika halfa ya kuadhimisha kifo cha mwanzilishi wa vuguvugu nchini humo Ayatollah Ruhollah Khomenei.
Awali aliishtumu Marekani kwa kujaribu kuhujumu benki za Iran, ambapo Makubaliano ya kinuklia kati ya Iran na mataifa sita ya magharibi yalisaidia kuinua vikwazo vilivyoathiri uchumi wa taifa hilo huku Tehran nayo ikikubali kudhibiti vitendo vyake vya kinuklia.
0 comments:
Post a Comment