Kupanda kwa kiwango cha mapato
miongoni mwa mataifa ya Afrika ni habari ya akawaida ,lakini wakati
huohuo watu hulalamika kwamba hawafaidiki.
Tatizo moja ni kwamba idfadi ya watu katika bara hili pia inaongezeka ikimaanisha kwamba kipato cha mtu mmoja hakiongezeki haraka.
Kuna swala la vle utajiri huo mpya unatumika.
Utafiti wa taasisi ya London ya Legatum ilioripotiwa na gazeti la Financial Times inasema kuwa kile ilichokitaja kwamba kimeimarika hakijaimarika katika mataifa mengi.
Ukuwaji wa uchumi unapimwa kulingana na kuimarika kwa sekta za biashara,Afya na elimu.
Mataifa kama kenya,Afika Kusini ,Rwanda,Mozambique na Cameroon yanayonekana kufanya vyema.
Lakini Nigeria ,angola na Sudan miongoni mwa mataifa mengine hayafanyi vyema.
0 comments:
Post a Comment