Operesheni kubwa ya uokoaji
inaendelea karibu na kisiwa cha Ugiriki cha Crete baada ya boti iliokuwa
na mamia ya wahamiaji kuzama.
Walinzi wa pwani ya Ugiriki wanasema kuwa zaidi ya watu 300 wameokolewa kufikia sasa huku miili mitatu ikipatikana.
Kiongozi wa shirika la kimataifa kuhusu Uhamiaji katika eneo hilo Daniel Esdras ameiambia BBC kwamba chombo hicho kilikuwa boti ya mita 25 kwa urefu ambayo ina uwezo wa kubeba watu 700.
Vyombo vya majini vya walinzi wa pwani ,ndege na helikopta zimehusishwa katika operesheni hiyo ambayo inafanyika yapata kilomita 100 kutoka pwani .
Hadi kufiki sasa ni wahamiaji wachache waliowasili Crete ambayo ipo kaskazini mwa Libya na Misri.
0 comments:
Post a Comment