Habari
njema! Baada ya staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’
kupewa kejeli nyingi za kutopata mtoto akipachikwa majina ‘negativu’
ikiwemo mgumba, mchungaji aliyetambulika kwa jina la Daudi Mashimo
amepata maono juu ya mlimbwende huyo na kuamua kukesha akimuombea apate
mimba.
NI WA KIUME KAMA SAMWELI
Akizungumza na Gazeti la Ijumaa mapema wiki hii, mchungaji huyo
anayeongoza kondoo katika Huduma ya Injili ya Maumivu na Uponyaji
iliyopo Mbezi-Msakuzi jijini Dar, alisema kuwa akiwa kwenye maombi
nyumbani kwake, siku moja majira ya mchana, alipata maono kutoka kwa
Mungu kwamba, ndani ya mwaka huu lazima Wema azae mtoto wa kiume.
Mchungaji Mashimo alisema kuwa, katika maono hayo, alioneshwa kwamba,
mtoto huyo atakuwa ni wa kipekee kwani atakuwa mtoto wa agano kama
ilivyokuwa kwa Samweli wa kwenye Biblia.
SIKU SABA ZA NAOMBI
Alifunguka
kwamba, baada ya maono hayo aliwashirikisha watumishi na baadhi ya
waumini wake hivyo wale waliokubaliana na maono hayo walitenga siku saba
ambapo walikuwa wakimuombea Wema usiku na mchana ili Mungu ampe mtoto
kama maono yalivyoonesha. “Wema amekejeliwa na kudhihakiwa sana, sasa
kupitia yeye Mungu anataka afanye muujiza, atampatia mtoto na Mungu
hasemi tu mtoto bali ni mtoto wa kiume, yaani atakuwa Samweli wa pili,
iwe ameolewa au hajaolewa, haijalishi. Ila ni kwamba Mungu amenionesha
hivyo. “Tumekuwa na maombi ya siku saba ya usiku na mchana hapa kanisani
(Mbezi-Msakuzi), tukimuombea Wema ili apate mtoto kama Mungu
alivyonionesha na naamini hilo linakwenda kutimia ili Watanzania wapate
sababu ya kumtukuza Mungu kupitia mwanadada huyo kwani Mungu amesikia
kilio chake,” alisema Mchungaji Mashimo.
USHUHUDA KWA TAIFA LA TZ
Mtumishi huyo alisema, kusudi la Mungu kumpa maono hayo ni kubwa
kwani Wema amekuwa akidharauliwa kwamba hazai hivyo haijalishi ni mchafu
kiasi gani ila Mungu atajiinua kwake ili watu waamini kuwa yupo na
hakuna linalomshinda kwa sababu mtoto wa kiume atakayezaliwa atakuwa wa
ushuhuda kwa Taifa la Tanzania.
WEMA: IPO SIKU NITAITWA MAMA Jitihada za kupata Wema kuzungumzia
maombi hayo yanayofanywa na mchungaji huyo kwa kushirikiana na waumini
wake hazikuzaa matunda ila kuhusu suala hilo la kupata mtoto, Miss
Tanzania huyo wa mwaka 2006/07 hivi karibuni alisema kuwa, watu wamekuwa
wakizungumzia ishu hiyo lakini anamuachia Mungu akiamini kuwa, ipo siku
naye ataitwa mama.
TUJIKUMBUSHE Wema amekuwa akipewa maneno mabaya ya kejeli kutoka kwa
watu mbalimbali kwamba hazai na hii ni baada ya yeye mwenyewe kuwahi
kukiri kuwa hawezi kuzaa kufuatia vipimo alivyofanyiwa na daktari wake.
Hata hivyo, miezi kadhaa iliyopita alikiri kuwa na ujauzito wa mpenzi
wake wa sasa, Idris Sultan ambao baadaye ulichoropoka. Katika sekeseke
la Wema kutopata mtoto, hivi karibuni, chipukizi wa Bongo Fleva, Rajabu
Abdulhan ‘Harmonize’ alidaiwa kumkejeli Wema kwa kusema kuwa hazai,
jambo lililomchukiza hata mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu ambaye
aliwaka akisema kuwa watu waache kumwandama mwanaye huyo
0 comments:
Post a Comment