Hivi
karibuni zilivuja taarifa kuwa, msanii wa filamu na muziki Bongo, Baby
Joseph Madaha ana kibendi ila kimeingia wakati hajajipanga hivyo anahaha
kutaka kukichoropoa.
Chanzo
makini kilicho karibu na staa huyo kilisema: “Huu ukimya wa Madaha ni
kwa sababu amenasa mimba lakini inavyoonekana imeingia bila kutarajia,
anachokifanya sasa ni kuangalia uwezekano wa kuichomoa.”
Baada
ya kupata ubuyu huyo, mwandishi wetu alimtafuta msanii huyo ili
kufungukia madai hayo ambapo alisema kuwa, asichuriwe kwani hana mimba
ila watu wanasema hivyo kutokana na kushiba tu.
“Mtu
akishiba tu, watu wanazusha una mimba, acheni kunichuria bwana, muda wa
mimi kupata mimba bado na ikiingia siwezi kuitoa,” alisema Baby Madaha.
0 comments:
Post a Comment