MC Pilipili kuwavunja mbavu Mbeya leo
MKALI
wa vichekesho vya jukwaani, Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ kwa mara ya
kwanza leo (Juni 3) anatarajiwa kuibukia Mbeya na kuwavunja mbavu wakazi
wa mkoa huo ndani ya Ukumbi wa Tugimbe Mafiati.
Akizungumza nasi, MC Pilipili
ambaye ni mkali wa vichekesho vya jukwaani alisema, shoo yake hiyo
itakwenda kwa jina la Cheka Vicheko vya Juu Nyanda za Juu na mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
“Natarajia kuandika historia kwa mara ya kwanza jijini Mbeya, sidhani kama kuna msanii wa vichekesho vya jukwaani aliyewahi kuweka rekodi ya kuchekesha, tukutane (leo) pale Tugimbe,” alisema MC Pilipili. Shoo hiyo itasindikizwa na mkali wa Bongo Fleva, Elius Barnaba
0 comments:
Post a Comment