Saturday, 4 June 2016

Mohammad Ali Afariki dunia.

Bondia wa zamani ambaye alijiita ‘the greatest’ ambaye alikuwa ni miongoni mwa watu maarufu na wenye wapenzi wengi duniani, Mohammad Ali amefariki akiwa na umri wa mika 74 kutokana na tatizo katika mfumo wa upumuaji.
Bingwa huyo wa dunia wa uzani wa juu wa zamani alilazwa hospitalini toka siku ya alhamisi June 02 2016 kufuatia tatizo kwenye mapafu, Bondia huyo mbali na kupatwa na tatizo hilo alikuwa akiugua kiharusi. Ali alipatikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka wa 1984 baada ya kustaafu ngumi za kulipwa . 

0 comments:

Post a Comment