Hatima
ya shauri lililofunguliwa na Chadema dhidi ya Polisi kupinga amri ya
kupiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa itajulikana Juni 21,
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza itakapotoa uamuzi kuhusu pingamizi
lililowasilishwa na upande wa utetezi kuomba litupiliwe mbali.
Jaji
Mohamed Gwae anayesikiliza shauri hilo, alifikia uamuzi huo baada ya
kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote za utetezi na mleta maombi.
Awali,
Mawakili wa utetezi, Robert Kidando na Obadia Kajungu waliomba Mahakama
kutupilia mbali maombi ya Chadema kuruhusiwa kufungua kesi
yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kwa madai
kuwa hayajakidhi mahitaji ya kisheria.
Akifafanua,
Wakili Kidando alidai mleta maombi hajataja baadhi ya vifungu muhimu
ikiwamo kifungu cha 5(1)(2), vinavyoipa Mahakama mamlaka ya kisheria
kusikiliza na kuamua maombi hayo.
Madai
hayo yalipingwa na mawakili wa Chadema; Gasper Mwanaliela na John
Mallya waliodai hoja za wajibu maombi hazina uhalali kisheria kwa sababu
hati ya maombi yaliyopo mbele ya Mahakama yamekidhi mahitaji ya
kisheria.
Wakili
Mallya alidai kisheria, hati ya maombi inapaswa kuwa na vitu vitatu
muhimu; hati ya kiapo, maelezo ya mleta maombi na ombi la shauri
kusikilizwa kama inavyoelekezwa na kifungu cha 5(3).
Wakili
Mallya aliomba Mahakama kutupilia mbali pingamizi la upande wa utetezi
na kumpa nafuu mleta maombi, kesi yake kusikilizwa na kuamuliwa.
Baada
ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Gwae aliahirisha shauri hilo
hadi Juni 21, Mahakama itakapotoa uamuzi huku akiuagiza upande wa
utetezi kuwasilisha hati kinzani kujibu hoja za mleta maombi.
Katika
maombi ya msingi, Chadema inaomba Mahakama kutamka kuwa amri ya polisi
na utekelezaji wake ni batili, kwa sababu ni kinyume cha katiba na
sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992.
Usikose Kufuatilia Dodosohabari.com
0 comments:
Post a Comment