MTUNZI:ENEA FAIDY
Ilikuwa
ni majira ya saa moja jioni ambapo mkuu wa while ya Mabango alikuwa
ofisini kwake akiwa amechanganyikiwa sana kwani hali ya shule hiyo
ilizidi kutisha sana hasa baada ya kutokea kwa vifo vya wanafunzi kumi
na tano mfululizo ndani ya wiki moja tu. Tena vifo vya ghafla tu.
Mkuu
wa shule mama Dayana Mbeshi alikuwa kwenye wakati mgumu sana kubaini
chanzo cha tatizo lakini bado hakupata majibu.Mara ghafla mlango wa
ofisi ukagongwa, akaingia mwalimu wa malezi wa shule hiyo akiwa na USO
wa huzuni sana hali iliyomshtua sana mkuu wa shule
"vipi kulikoni?"
"hali mbaya mkuu.. wanafunzi wawili wamefariki tena bwenini" mwalimu wa malezi alizungumza kwa huzuni iliyochanganyika na hofu.
"what?
mmh! sio bure.. kuna kitu hapa..!" alisikika mwalimu Mbeshi huku
akiinamisha kichwa chake chini na kukiegemeza kwenye kiganja chake.
******
Wanafunzi
wengi walionekana kuwa na hofu sana baada ya vifo visivotarajiwa kuzidi
kutokea katika shule yao. Kila MTU aliwaza sana juu ya vifo vile huku
kila mmoja akihisi zamu yake IPO karibu. Nyuso za huzuni ndizo
zilizotawala kwa wanafunzi wote si wa kike
wala wa kiume. Hakuna aliyetamani kulala wala kukaa mbali na kundi la
watu kwani hofu iliwajaa mioyoni mwao, hawakuweza hata kusoma.
Lakini
hali ilikuwa tofauti sana kwa binti Doreen ambaye alikuwa na wiki tu
toka ahamie shuleni hapo. Alionekana kutoogopa chochote wala kuguswa na
misiba ya wanafunzi
wenzake. Kila Mara alionekana akiwa na furaha, hali hii iliwatisha
wanafunzi wenzake na kuwafanya wawe na maswali mengi juu yake.
Doreen alikuwa msichana mrembo, sura yake
nyembamba iliyopambwa na macho makubwa legevu, kope ndefu nyeusi tii,
pua nyembamba iliyochongoka vyema na midomo mizuri yenye mvuto wa aina yake vilimfanya awe tishio kila kona kwani alikuwa ni mzuri kupindukia lakini Tabia ilikuwa tofauti na uzuri wake.
Wakati
wanafunzi wengine wakiwalilia wenzao Doreen alikuwa amejitenga peke
take nyuma ya bweni alilokuwa anakaa na kulikuwa na Giza totoro. Alikuwa
uchi wa mnyama huku mikono yake ikiwa imeshikilia vitu fulani huku akitamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe....
Itaendelea.......
Itaendelea.......
0 comments:
Post a Comment