Saturday, 18 June 2016

Sherehe za kimila zenye asili ya ukeketaji zapigwa marufuku wilayani Longido.


Sherehe zote za kimila zenye viashiria vya kutekeleza vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike vimepiga marufuku katikaTarafa ya ketumbeine iliyopo wilayani longido.
 
Uamuzi huo unatolewa  na Afisa wa tarafa hiyo Bwana Pamphili Oduka mbele ya wazazi na watoto kutoka maeneo mbalimbali ya tarafa hiyo walikutana kwenye maadhimisho ya mtoto wa Afrika baada ya kubainika kuwa vitendo vya ukeketaji vimekua vikiendelezwa kwa siri kwa visingizio vya sherehe za kimila.
 
Tatizo la ukeketaji sio pekee linalowatatiza watoto wa kike wilayani Longido kwani lipo tatizo la mimba za utotoni ambalo Afisa maendeleo ya jamii,jinsia na watoto wa halmashauri ya wilaya hiyo Atuganile Chisonga anasema katika kipindi cha mwaka huu tu tayari watoto nane wa kidato cha kwanza wamekatiza masomo.
 
Shirika la kimataifa la World Vision Tanzania ni wadau wanaoshughulika na haki za watoto wilayani humo wanasema suala la msingi linalohitajika ni wadau ni kubadili fikra za wanajamii hao

0 comments:

Post a Comment