Wadau wa elimu wanasema matokeo ya serikali kupanga bajeti finyu katika sekta ya elimu kumechangia ongezeko la umaskini na mgawanyo wa rasilimali usiokuwa na usawa katika jamii.
Mratibu wa mtandao wa elimu nchini TANMET Bi CATHLEEN SEKWAO
amesema hali hiyo itaepukika tu endapo serikali itaongeza bajeti kwa
ujumla hasa kwa watoto wenye mahitaji maalumu na waliopo katika shule
jumuishi.
Alikuwa akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya elimu duniani
kitaifa yaliyofanyika Kilwa Masoko Mkoani lindi ambayo yaliyoambatana na
maandamano yenye ujumbe mbalimbali.
Kwa upande wao wadau wa elimu wamesema takwimu zinaonyesha kuwa
hali ya elimu nchini bado hairidhishi kutokana na takwimu kuonyesha bado
kuna idadi kubwa ya watoto wa shule za msingi hawajui kusoma na
kuandika.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na
Ufundi Mkaguzi wa Elimu wilaya ya kilwa TABU NASSORO amesema serikali
inatambua mchango wa wadau wa elimu, taasisi na sekta binafsi katika
kutatua changamoto za elimu nchini hivyo itaendelea kutoa ushirikiano.
0 comments:
Post a Comment