Hayo yamebainishwa na matokeo ya utafiti uliofanywa na Baraza la
Kilimo na Mifugo Tanzania kwa kushirikiana na wataalamu kutoka chuo
kikuu cha Daresalaamu katika wilaya kumi hapa nchini.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa baraza hilo CLEOPHAS RWECHUNGURA
na mtaalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam KHALID FWADILI mkoani
Njombe mavuno ya mahindi yanashuka kwa wastani wa asilimia 4.3 hali
inayoporomosha uchumi wa wakulima.
Katika mdahalo wa mbegu bandia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye
pia ni Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bwana ANATOLY CHOYA amesema juhudi
zinafanyika kupambana na wauzaji na waagizaji wa pembejeo bandia.
0 comments:
Post a Comment