Shirika
la Umeme liko hatua za mwisho Mkoani Morogoro kukamilisha miradi
mikubwa ya umeme, ukiwemo mradi wa umeme mijini na ule unaofadhiliwa na
mradi wa umeme vijijini REA ambapo zaidi ya watu 11,300 wanatarajiwa
kufikiwa na umeme.
Hatua hiyo inakuja wakati Serikali ikielekeza nguvu zake katika
mapinduzi ya Uchumi kupitia viwanda na huku fursa zaidi za kiuchumi
zikiendelea kujitokeza kufanikisha azma hiyo mkoani kuchangia sekta ya
viwanda.
Mhandisi wa umeme David Chisot anayeshughulikia masuala ya Ujenzi
na miundombinu ya umeme toka shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Morogoro,
amesema kupitia miradi hiyo,wateja wakubwa na wadogo wataweza kufikiwa
na nishati ya umeme katika maeneo ambayo awali hayakuwa na umeme
kabisa.
Chisot amesema miradi inayofadhiliwa na REA inayogharimu
itahusisha wilaya 4 katika mkoa wa Morogoro ikiwemo Morogoro katika
vijiji 27 , Mvomero vijiji 35, Kilombero vijiji vinne na Ulanga vijiji 5
vitano ambapo tayari wateja 5,562 wa mradi wa REA wameanza kunufaika
na mpango huo wakiwemo wateja wadogo 5457 Na wakubwa 205.
0 comments:
Post a Comment