Saturday, 21 May 2016

kutenguliwa kwa kitwanga kumefuata taratibu za utumishi wa Umma


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani,Bw.Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.
Ametoa ufafanuzi Ijumaa,Mei 20,2016 wakati akijibu swali la mwandishi wa TBC1 aliyetaka kujua kama taarifa zilizoenea kuhusu kutenguliwa kwa Waziri huyo ni za kweli.
 
Waziri Mkuu amesema kuna swali aliloulizwa ambalo hakulijibu vizuri na kwamba swali hilo litapaswa kurudiwa kuulizwa baada ya wabunge kuomba muongozo wa swali hilo.

0 comments:

Post a Comment