Friday, 20 May 2016

Ujenzi reli ya kisasa kuanza.


UJENZI wa reli ya kati ya kisasa (standard gauge) unatarajiwa kuanza kwa kilometa 1,219 na mchakato unaendelea ili kupata mzabuni.

Wakati reli hiyo ina jumla ya kilometa 2,527 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza na Kigoma, zinazotarajiwa kuanza kujengwa ni njia ya kutoka Dar es Salaam-Tabora-Isaka-Mwanza ambazo ni kilometa 1,219.

Kilometa ambazo zitasubiri kutokana na kile kilichoelezwa kuwa haiwezekani kujenga mradi kwa pamoja kutokana na gharama kubwa ni Tabora –Kigoma (kilometa 411), Uvinza –Msongati (200), Kaliua –Mpanda-Kalema (360) na Isaka –Lusumo kilometa 337.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alifafanua kwamba uamuzi huo, unatokana na gharama za ujenzi wa reli yote kuwa kubwa na hivyo kutakiwa kuwa na Sh trilioni 16.

Mbarawa alisema hayo juzi alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati akihitimisha mjadala wa bajeti yake.

“Ikiwa kama nchi inataka kujenga mradi huu kwa pamoja, inahitajika kuwa na dola bilioni nane sawa na trilioni 16 (shilingi) ambazo ni pesa nyingi na hakuna nchi inayoweza kutoa mkopo huo,” alisema

0 comments:

Post a Comment