Friday, 20 May 2016

DARASA LA UHUSIANO, JE WANAUME WANAPENDA NINI KATIKA MAPENZI.


Sometimes Wanawake huwa wanajiuliza Maswali mengi,wafanyeje ili wapendwe,wanahisi wana bahati mbaya,kila wanapojitoa mioyo yao inaumizwa.Jamaa hawakai,wanatupia kitu,wanakula mzigo wanatembea na Bwana..Mioyo yao imejaa matundu na hawaamini kabisa kama Wanaume huwa wanapenda,imefikia point wanadhani Wanaume hutamani tu kumbe SI KWELI!

Wanaume nao wana taste zao,hawaendi tu kama Mbwa koko,jalala moja baada ya jingine,HAPANA...Know their taste and you will enjoy theirs.

Sifa za Mwanamke ambae Mwanaume atavutiwa na kukaa ni hizi zifuatazo,JITAZAME,kama huna any of these,you better try to learn to have them,its not too late:

1.MWANAMKE MWENYE MSIMAMO
Jambo moja muhimu,the number 1 thing ambacho Mwanaume anaangalia kwa Mwanamke ni Msimamo wako...Sio Mwanamke uko kama Feni,kila sehemu unapulizia upepo,Mashariki,Magharibi kote wewe...Hapo sahau,tena sahau sana.Mwanaume anahitaji kuwa na uhakika,Mwanamke aliyemkabidhi moyo hana mishemishe na hayumbishwi na lolote,na chochote na penzi lake liko safe
Unaweza kuwa na kila kitu,Mzuri wa Sura na kila kituuuu,na bado usimpate Mwanaume wa Maana kama huna sifa hii,hakuna muujiza kwenye hili,ndo wanaume walivyoumbwa,if you lack this hamna Mwanaume wa Maana utapata,utapata vimeo kama ulivyo!

2.MWANAMKE MUELEWA
Men are simple creatures,they love to live simple,and take them simple as they are...
Ukiwa aina ya Mwanamke unamind vitu...kitu kidogo ugomvi...Unaongea na nani...Uko wapi..Na nani,Kwanini,hee,jamanikama Mahaakama kuu??Hapa unapoteza Credits

Kuwa aina ya Mwanamke muelewa ambae utamfanya Mwanaume ajisikie vibaya kufanya kitu flani ambacho ulishamwambia asifanye before...Lakini sio kukaripia na kununa kwa sababu amerudia..let him realize that amefanya kitu cha kukuudhi na hujareact,and if hes aman enough,he will know and apologize
Ila kama ni gumegume basi tena,litakausha na ndo inakuwa issue hapo...Are u patient enough to handle it??kazi kwako,ila kuna wanawake wana uwezo huu,learn from them wamewezaje..No matter how complicated the man is,they know how to handle him

Jua Lugha ya kutumia ambayo utafikisha ujumbe and yet you dont show him kwamba umemind na unamkaripia...kumkaripia Mwanaume ni msala mpya,hata kama ana kosa atakumind na itakula kwako...Una ulimi mzuri kufikisha ujumbe??

3.MWANAMKE DIRECTOR
Baba ni kichwa cha nyumba....mimi huamini Mama ni macho yaliyo kwenye kichwa hicho
Women play a very vital role in DIRECTING THE HEAD TO THE RIGHT WAY
Kichwa bila macho si utajigonga tu????Mwanamke ni jicho...

Ukikalia kujiremba tu na kuwaza mambo mengine bila kujua kuna kichwa kinasubiri maelekezo yako,utaonekana bogus..kutwa uko kwenye Umbea,huna muda wa kujua ur man anafanya nini,ana plan gani mwaka huo,unamsaidiaje kuzifikia,sasa we faida yako nini kwenye maisha yake??
be the kind of a woman ambae Mwanaume aki-achieve jambo anasema I have a woman beside of me who engineered this...Kama hujawahi kufikia hatua ya kuwaappreciated na ur man kwa jambo hili jua kuna mahali umefeli...Na hili haliji hivihivi,linakuja pale kunapokuwa na proper communication between you and ur man...Bila good communication:

1.Hutajua what ur man is up to

2.Kwa sababu hujui what he is up to hutakuwa na msaada.

3.Akifaulu,jua haupo kwenye picha ya mafanikio yake na ur simply useless

4.Akifeli,ur part of his failure kwamba humsaidii lolote..ur simply useless and actually absent in his life kwa sababu uwepo wako haumsaidii its better he becomes alone!YOU HEARD???

Women have planning and control ability,USE IT...Usikae tu kama muuza genge unasubiri wateja,Do your job and Win him!

4.MWANAMKE MSAFI NA MZURI
Usafi huu sio wa nguo tu na kunukia,ni zaidi ya hilo...

Usafi unaanzia ndani..Msaidie Mwanaume awe msafi pia,rohoni hadi mwilini...Rohoni how???Jitu halisali,halikumbuki kuna Mungu,lipo tu,unadhani mtajenga Familia gani baadae???

Msaidie kum-remind kukumbuka hilo,Mafanikio ya nje huanzia ndani..Dirty inside,Dirty Outside...Mambo mengine anafanya nje na yanaku-affect kwa sababu umefeli ku-inspire change ya ndani...Ngumu hii lakini ndo hivyo..You cansave a lot of energy kama atakuwa msafi wa ndani,everything outside will be set automatically...Whatever u see in physical started in Spiritual...Yeah right! Hata ulimwengu uliumbwa,na vyote unavyoviona baada ya Plan ya Spirit kumalizaika.Soma Kitabu cha Mwanzo kwenye Biblia,uone Uumbaji ulifanyikaje...Same applies na hapa,Uumbajiwa vitu vya nje,Mahusiano imara,Familia bora,inajengwa ndani..

Sio kazi yako ni kuuliza Baby hatuendi Club,Baby this...Unamkumbusha kusali???Utatengeneza mme freemason bila kujua...Mtu hasali we upo tu unaona sawa...CHANGE!

Huu usafi mwingine wanawake mmejaliwa,biashara za kunuka kikwapa no,Kusafisha nyumba vema saafiii...mengine si kama kawa??Mpango mzima uko hapo.

Uzuri huwa ni subjective...Unaweza kuwa mzuri kwangu lakini ni wa kawaida kabisa kwa mwingine....Ukiwa msafi unaweza ukamfanya Man wako aone potential,hata kama wewe sio mzuri sana lakini anaona Kiongozi wa Familia inside you and he will definitely opt you.
Hamna limbwata wala nini,tupa kule mbali...

Kama huna hizi sifa 4,aisee waza upya...Unaweza bahatisha ndulute ukaolewa,lakini jusitegemee muujiza,gomalitapata Pancha tu...Jamaa hataweza kukaa na nunda...Atajutia Mahari aliyolipa ila atasepa kimyakimya..

To avoid that,please make sure you do your Homework well ili Mtihani ukija unafaulu tu bila shida...
Jitathmini halafu KAA HUMO!

0 comments:

Post a Comment