DIWANI wa Kata ya Bahi, Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma, Agustino Ndowo ameitaka serikali kuingilia kati ujenzi wa kisima cha maji katika kijiji cha Uhelela wilayani humo ambacho kilitoa maji siku moja tu huku wakimtafuta mkandarasi wa mradi huo bila mafanikio.
Akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani ambaye alitembelea Wilaya hiyo juzi, Ndowo alisema kisima hicho kilijengwa mbadala wa kisima walichokuwa wakitumia awali wananchi hao ambapo sasa eneo hilo limepitiwa na umeme wa msongo mkubwa.
Amesema baada ya kisima cha awali kupitiwa na umeme Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) waliamua kuwafidia wananchi kisima kingine lakini cha kushangaza kisima kipya kiliwahi kutoa maji mara moja tu hadi sasa ambapo wananchi wamekuwa wakitumia maji ya madimbwi ambayo si salama huku mkandarasi wa mradi huo akiwa haonekani.
“Maji yalitoka siku moja tu na mpaka sasa kisima akifanyi kazi mkandarasi haonekani, tunataka pia thamani ya mradi iwekwe wazi kwa nini wanafichaficha” alisemaKwa upande wake Mbunge wa Bahi Omar Baduel alisema awali kulikuwa na kisima cha kijiji lakini Tanesco walipopitisha umeme wa msongo mkubwa wananchi wakatakiwa wasiendelee kutumia kisima kile kwa usalama wao.
Alisema wananchi wamekuwa wakidai kuwa kisima kinachojengwa hakina ubora kama kile cha awali, ambapo Akijibu hoja hizo Naibu Waziri alisema wanaendelea na juhudi za kumtafuta mkandarasi wa mradi huo.
“Kuna mkandarasi aliyepewa kufanya kazi hiyo ila hajapatikana tunaendelea kumtafuta na nimeshawaeleza Tanesco hadi Juni 30 kisima hiki kiwe kinafanya kazi” alisema
Alisema amefanikiwa kuongea na mwenye kampuni ya ukandarasi waliopewa kazi ya ujenzi wa kisima hicho na kumtaka kufika Dodoma kujieleza na tujui alilipwa Sh.ngapi kwa ajili ya ujenzi wa mradi.
“Hata hili tenki wameliweka chini badala ya juu sasa maji yatapandaje hapo” alisemaAliwataka wananchi kuondoa hofu kwani suala hilo linashughulikiwa na watapata maji kama kawaida baada ya kazi kukamilika.
Wednesday, 18 May 2016
Home »
Habari
,
Kijamii
» SERIKALI YAOMBWA KUINGILIA MGOGORO WA UJENZI WA KISIMA CHA MAJI KATIKA KATA UHELE WILAYANI BAHI.






0 comments:
Post a Comment