Friday, 20 May 2016

Biashara Za Donald Trump Zaongeza Mapato Mengi Zaidi.


Mgombea Urais wa Marekani Donald Trump.
Mapato ya biashara za Donald Trump yameongezeka kwa dola milioni 190 tangu tajiri huyo kuwania urais wa Marekani kulingana na nakala mpya za kifedha.
Wito wake wa kuwazuia Waislamu kuingia nchini Marekani pamoja na kuwafurusha mamilioni ya wahamiaji wasio na vibali haukuathiri biashara zake.

Kampuni kadhaa zilivunja uhusiano wake na bw Trump wakati alipozindua kampeni yake.

Kitabu chake cha hivi karibuni ,Crippled America,kilipata kati ya dola milioni 1 na 5 ya mrahaba,kulingana na Trump.
 
Mapato yaliongezeka maradufu katika hoteli ya Mar-a-Lago iliopo mjini Florida kutoka dola milioni 16 hadi milioni 30.kampuni yake ya maji ,Trump Ice pia ilikuwa.

0 comments:

Post a Comment