Akiwasilisha taarifa hiyo ya mwaka wa fedha ulioishia Juni 2018 leo ofisini kwake jijini Dodoma,profesa ASSAD ametaja baadhi ya makampuni hayo kuwa ni kampuni ya ndege Tanzania ATCL,baraza la michezo la Taifa,Mamlaka za maji safi na Usafi wa Mazingira Lindi,Shirika la Maendeleo ya Petroli(TPDC) na bodi ya Utalii Tanzania.
Mashirika mengine ni Shirika la Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam(DAWASCO),kampuni ya Maendeleo ya Nishat ya Joto Tanzania(TGDC),Baraza la Taifa la Biashara,Bodi ya Maziwa Tanzania na mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam(DAWASA).
Akizungumzia matokeo ya kaguzi maalum uliofanywa na ofisi yake profesa ASSAD amesema umebaini kuwa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umelipa malipo hewa ya shilingi bilioni 2.61 kwa mzabuni.
Kutokana na hilo amependekeza hatua stahiki za kisheria na kinidhamu zichukuliwe dhidi ya maofisa waliohusika katika ubadhilifu wa mali za umma na mamlaka husika zihakikishe mianya yote iliyobainishwa wakati wa ukaguzi inayopelekea upotevu wa mali inazibwa.







0 comments:
Post a Comment