Waziri wa chi ofisi ya makamu wa rais ,muungano na mazingira Mh:January Makamba amesema ,katazo
la matumizi ya mifuko ya plastic siyo la kuhtukiza.
Makamba ameyasema hayo hii leo katika mkutano na
waandishi wa habari uliyofanyika mkoani Dodoma,huku akifafanua juu ya njia mbadala
itakyotumik
Makamba amewaambia
waandishi kuwa ifikapo mwaka 2050 kutakuwa na taka nyingi ya
mifuko hiyo kuliko wingi wa samaki katika bahari na maziwa .
Marufuku ya utengenezaji,
usambazaji na matumizi ya mifuko hiyo itakayoanza rasmi juni mosi mwaka huu ,itaambatana
na kanuni mpya itakayotungwa chini ya sharia ya mazingira.
Mkutano na waandishi wa habari umekuja siku moja baada ya waziri mkuu Kasim Majaliwa Kusema kuwa wanafanya hivyo ili kulinda afya ya jamii,wanyama ,mazingira na miundombinu dhidi ya athari itokanayo na taka za plastiki.,







0 comments:
Post a Comment