SERIKALI imesema
idadi ya watumiaji simu imeongezeka kutoka watu milioni 17.6 kwa mwaka
2009 hadi kufikia watumiaji milioni 43.6 kwa mwaka 2018.
Ongezeko hilo
limechangiwa na juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali ikiwemo ujenzi wa
Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na kuunganisha na Mikongo ya Baharini ya SEACOM
na EASSy.
Takwimu hizo
zimetolewa leo jijini Dodoma na Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano
mhandisi ATASHASTA NDITIYE wakati akifungua kikao cha serikali,sekta binafsi na
sekta ya elimu ya juu na ufundi leo jijini Dodoma.
Mbali na
mafanikio hayo amesisitiza suala la kutekelezwa maelekezo aliyoyatoa mwaka jana
ya kuwatambua wahitimu na wataalam wa TEHAMA kwa weledi wao ili watambuliwe kwa
urahisi wakati wa kuingia katika soko la ajira.
Kwa upande wake
kaimu katibu mkuu wa wizara hiyo Dokta JIM YONAZI amesema lengo la kikao hicho
ni kuwa na uelewa wa pamoja wa Sera ya Taifa ya TEHAMA.
Nae mwakilishi
wa sekta binafsi MGETA MJUNGU ametaja changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta
hiyo na kusisitiza suala la ushirikiano baina yao na serikali.
Kauli mbiu ya
mkutano huo inasema TEHAMA ni nguzo ya Maendeleo ya uchumi wa Viwanda wa
Tanzania.









0 comments:
Post a Comment