Mkuu wa masuala ya haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet, amesema majaji na maafisa wanaotunga sheria duniani wanahitaji kupata mafunzo maalum ya kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake.
Bachelet amesema ikiwa leo dunia inaadhimisha Siku ya Wanawake, anatoa wito wa dharura kwa serikali, wabunge na mahakama duniani kote kuongeza kasi katika harakati za kijamii za kupambana na unyanyasaji wa kijinsia.
Amesema polisi na maafisa wa mahakama lazima wapewe mafunzo ya kuondoa unyanyasaji wa kijinsia. Wakati Bachelet akitaka wanawake wapewe nafasi za juu katika kutunga sheria na sera ambazo zinawahusu, pia ameelezea mafanikio ya jumla katika haki za wanawake.
Amesema katika kipindi cha miezi sita iliyopita, wanawake wameshika nafasi za juu kisiasa kwenye nchi za Ethiopia, Tunisia, Costa Rica na Marekani na wametetea waziwazi uwezeshaji kwa wanawake na usawa wa kijinsia.
Chanzo DW
0 comments:
Post a Comment