Takriban asilimia 60 ya watu wamefikiwa na huduma ya
maji safi na salama ,huku asilimia 46.24 wakifikiwa na kiwango cha vyoo bora
vilivyoboreshwa.
Taarifa hiyo iliyojiri juma lililopita wakati wa
kilele cha wiki ya maji na imefafafanua kuwa idadi ya watu inakua kwa kiasi
kikubwa na kuzidisha athari zitokanazo na upungufu wa huduma za usafi wa mazingira.
Hata hivyo mahitaji ya maji katika secta za
uzalishaji mf.umeme ,kilimo ,utengenezaji
wa viwanda yanakuwa kwa kasi kadiri uchumi unavyokuwa na hivyo kutajwa kuwa
secta hiyo itaendelea kukua iwapo msukumo ukiwekwa kwenye rasilimali hiyo ya asili kwa kadiri idadi ya watu inavyokua.
katika dhamira ya hakuna anaye achwa nyuma ,serikali ,secta binafsi ,taasisi za
kitaaluma na asasi zisizo za kiserikali hukutana kubadilishana ujuzi
,kutathimini ufanisi na kuandaa ufumbuzi wa changamoto zinazohusiana na maji
katika juhudi za kuhakikisha hakuna yeyote anayeachwa nyuma.
Aidha,Huduma za usafi zilizoboreshwa zimetajwa kuifanya
Tanzania kuokoa kiasi cha dola za kimarekani milioni milioni 206 kwa mwaka au
1% ya GDP.
Taarifa hii inajiri wakati ambapo ni siku nne
zimepita tangu Tanzania kuungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha wiki ya
maji ,ambapo kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika jijini Dodoma







0 comments:
Post a Comment