Shirika lisilo la serikali la ECLAT Foundation la wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara limeahidi kujenga madarasa matatu katika shule mpya ya sekondari Songambele ya mji mdogo wa Mirerani ambayo ina wanafunzi mia mbili (200) wa kidato cha kwanza ili kupunguza mrundikano darasani.
Akizungumza kwenye kikao cha mamlaka ndogo ya mji wa Mirerani mwenyekiti wa shirika hilo Peter Toima amesema lengo lao ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kuleta maendeleo.
Ni kuweka tu utaratibu sasa kwamba katika kazi hii katika Amesema kwa sasa kilichobaki ni kushirikishana kwa pamoja na Mamlaka ya mji mdogo huo na kujua ni kitu gani ambacho kinatakiwa kufanyika kwa sasa ili kuikamilisha shule hiyo.
Ameongeza kuwa Shule hiyo mpya ya Sekondari Songambele yenye vyumba vitano vya Madarasa iongezewe nguvu haraka katika kuongeza majengo mengine ili kuwnusuru wanafunzi wajao kukosa madarasa kwa ya kusomea.
Naye mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani Adam Kobelo amesema shule itasaidia kuwapunguzia wanafunzi umbali wa kilomita ishirini [20] wanazotembea kila siku kufuata elimu.







0 comments:
Post a Comment