Tuesday, 19 March 2019

Makada walio nje ya Tarime watakiwa kurudi ili kufanya maendeleo

Makada walio nje ya Tarime watakiwa kurudi ili kufanya maendeleo

Makada wa Chama cha mapinduzi walio nje ya Tarime  mkoani Mara wametakiwa kurejea Nyumbani Tarime kwa lengo la kuunga juhudi zinazofanywa na jamii za maendeleo.

Akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake katibu wa Chama cha mapinduzi CCM Wilaya Tarime mkoani Mara,Khamisi Mukaruka alisema kuwa kuna haja Makanda wa Chama hicho kukumbuka Nyumbani na kurejea kuja kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanyika.

“Ndugu zangu niseme kuwa kwasababu siasa ndani ya wilaya Tarime sio nzuri ambapo halmashauri zote mbili zinaongozwa na Chama pinzani (Chadema) kwa hali hiyo tunawaomba Makanda wote walionje ya Tarime kurudi na kuja kuunga juhudi za maendeleo zinazofanyika na hiyo itatusaidia kukomboa majimbo hayo katika uchaguzi ujao”alisema Mukaruka. 

Mukaruka aliongeza kuwa Chama kama Chama kinawakaribisha Makada mbalimbali walionje ya Tarime wanaowiwa na maendeleo kuja kuunga juhudi za Rais John Pombe Magufuli katika kutekeleza maendeleo kwa wananchi wake.

Naye Mweyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi UVCCM Wilaya Tarime,Godfrey Fransice alisema kuwa hali ya Siasa kwa wilaya Tarime kwa sasa wanaasilimia kubwa ya kushinda Chama cha mapinduzi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na kuchukua viti vingi pamoja na uchaguzi mkuu ujao wa Urais,Ubunge na Udiwani.

Fransince aliongeza kuwa Waandishi wa habari wanatakiwa kuunga mkono na kutangaza shuguli za maendeleo zianazotekelezwa na Chama hicho kwa wananchi wake bila kupendelea

0 comments:

Post a Comment