Kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana U17 Serengeti Boys wakiwa kwenye mazoezi mepesi kwenye Uwanja wa Tennis. Serengeti Boys wapo nchini Uturuki kwenye mashindano ya Kimataifa ya UEFA ASSIST.
Katika michuano hiyo nchini Uturuki, Tanzania imepangwa Kundi A pamoja na Guinea, Australia na wenyeji, Uturuki, wakati Kundi B linaundwa na timu za Cameroon, Uganda, Morocco na Belarus na Kundi C lina timu za Senegal, Nigeria, Angola na Montenegro.
Tanzania inatumia michuano hiyo kama maandalizi yake ya mwisho ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) ambayo wao watakuwa wenyeji kuanzia Aprili 14 hadi 28 mjini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment