Saturday, 9 March 2019

Sababu za malengo yako kutokutimia

Sababu za malengo yako kutokutimia

Watu wanakuwa na shauku kubwa ya kupanga na kutekeleza mipango yao lakini mipango mingi haitekelezwi. Sababuni nini? Utajiuliza. Katika makala hii tutaangalia sababu kubwa zinazofanya malengo ya mwaka yasikamilike.

Sababu Kuu  Kwanini Mipango na Maazimio ya Mwaka Mpya Hayafanikiwi:

Kutaka Kufanya Mambo Mengi kwa Mara Moja.
Kutaka malengo ya maisha yako yote au ya miaka 10 yafanyike katika mwaka mmoja,ni jambo lisilowezekana. Na wengi tunashindwa hapa.

Ni lazima kuangalia uwezo wakutekeleza mipango hiyo katika kipindi husika. Malengo mengi tunayoweka ni matamanio yetu katika maisha. Ni vitu ambavyo tungependa vitokee au tuvikamilishe katika maisha yetu.

Kutokuwa na Mpango wa Utekelezaji
Kila lengo ni lazima litengenezewe mpango wa kulitekeleza. Hapa utavunjavunja kila lengo katika kazi ndogondogo na kuzipangia muda kwa kila kazi pamoja na muhusika (nani atakayefanya) na mahitaji yake ya kuikamilisha.

Lengo linaweza kuwa kubwa sana na lisilotekelezeka mpaka utakapoweza kulikatakata katika vipande vidogo vidogo.

Kukosa mkazo na msukumo
Hili linaweza kutokea ukiwa na malengo mengi kupita kiasi. Ambapo utashindwa kutulia katika lengo moja na kupata matokeo. Badala yake utakuwa unafanya nusu ya hili na nusu kwingine pia na hatimaye hutatimiza hata moja.

Unapokuwa hufanikishi kazi yoyote unakosa msukumo wa kufanya mengine pia na kufa moyo.

Kutoandika na kutorudia kuyasoma malengo yako
Iwe unaandika au unatunza kichwani ni muhimu sana kuyarudia malengo yako kila mara. Wataalamu wanashauri uyasome kila siku asubuhi ,mchana na jioni.

Tembea nayo kila unakoenda na kamwe usiachane nayo. Unaporudia kusoma malengo yako yanawekwa kwenye mawazo au akili ya kina  ambayo inauwezo mkubwa wa kukusukuma kukamilisha malengo hayo.

Kutoshirikisha Wengine.
Njia nyingine ni kushirikisha wengine, mfano mwenza wako au marafiki au wazazi n.k. Hawa watakukumbusha pale unapojisahau. Mipango ya mtu mmoja haina nguvu na ni rahisi kuiacha kabla ya kufikia mwisho. Pale unapowashirikisha wengine mwili na akili yako inakuwa imejipa jukumu ya kuhakikisha inatimiza,linakuwa kama deni kwako ambalo ni lazima ulilipe.

Kutopima maendeleo mara kwa mara
Ni muhimu kuyapitia malengo yako na kuyapima mara kwa mara. Angalia kila baada ya mwezi mmmoja mfano,je umefikia wapi? Na kama siyo,changamoto ni nini ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi na kuweza kwenda mbele.

Bila shaka makala hii itakupa mwanga na mwongozo pale unapoandika maelengo yako ya mwaka mpya ili hatimaye ufanikiwe kwa kuyatimiliza.

Nakutakia heri na mafanikio kwenye mipango yako mipya ya mwaka.

0 comments:

Post a Comment