Mhandisi apewa siku nne Wananchi wapate maji
Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Bahi Hafidhi Juma ameagizwa na Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso kuhakikisha ndani ya siku nne Wananchi wa Kijiji cha Mkakatika, kata ya Mpamantwa wilayani humo wanapata huduma ya maji safi na salama.
Naibu Waziri Aweso amefikia uamuzi huo wakati akikagua miradi ya maji inayotekelezwa na serikali ndani ya Wilaya ya Bahi, na kukuta kijiji cha Mkakatika ulipomradi wa maji lakini wananchi wanakosa maji kwa kukosa tanki la kuhifadhia maji.
Aweso amemtaka mhandisi wa maji Wilaya ya Bahi kuhakikisha ndani ya siku nne awe amepeleka tanki kwa ajiri ya kuhifadhia maji ili wananchi hao waweze kupata maji safi na salama.
“Nikuagize Mhandisi ndani ya siku nne muwe tayari mmeshanunua tanki la maji na wananchi wanapata maji haiwezekani mshindwe kununua tanki la milioni moja au msubiri serikali ilete hapana, nawapa siku nne muhakikishe tanki linafika hapa na wananchi wanapata maji,” amesema
Naibu Waziri Aweso pia amemuagiza mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamis Mkunda, kuvunja kamati ya maji ya kijiji hicho kwani imeshindwa kusimamia mapato ya maji hali iliyopelekea kukosa fedha za kununulia tanki mpya la maji pindi tanki lilipoharibika.







0 comments:
Post a Comment