Rais Uhuru Kenyatta uzuru Rwanda na Uganda licha ya mzozo baina yao
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amefanya ziara ya siku moja nchini Rwanda ambako amekuwa na mazungumzo ya faragha na mwenzake Paul Kagame.Lengo la ziara hiyo halikuwekwa wazi.
Rais Kenyatta pia amekutana na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni alipokuwa njiani kurejea nyumbani kutoka Rwanda.
Ziara ya Rais Kenyatta inakuja wakati kukiwa na mvutano kati ya Rwanda na Uganda unaonekana kuzidi kuendelea.
Rwanda inailaumu Uganda kwa kufanya njama dhidi yake huku Uganda nayo ikipinga vikali madai hayo.
Rais Kenyatta, alisema ziara yake ni ya kuimarisha uhusiano lakini wadadisi wa kisiasa wanasema ni juhudi za chini kwa chini za upatanishi au kutafuta suluhu ya jinsi ya kutatua mgogoro baina ya Rwanda na Uganda.
Mzozo kati ya mataifa hayo mawili uliifanya Rwanda kufunga mpaka wake na Uganda uliyo na shughuli nyingi.
![Rais wa Rwanda Paul Kagame](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/4F64/production/_105942302_1fe44d70-9e22-4d6e-93a4-130a5f998dfe.jpg)
Hatua ambayo kamishena wa forodha wa mamlaka ya kutoza ushuru nchini Uganda, Dicksons Kateshumbwa,anasema ilikuwa na athari kwa Kenya.
Siku moja iliyopita Rais Kagame alielezea kwa mara ya kwanza alielezea chimbuko la mgogoro baina ya nchi yake na Uganda akisema ulizuka tangu miaka 20 iliyopita wakati Uganda ilipotaka kuangusha utawala wake.
Rais Kagame alisema mgogoro huo ulishika kasi mnamo miaka ya hivi karibuni kutokana na serikali ya Uganda kuunga mkono kundi la RNC linalopinga Rwanda na ambalo linatumiwa na Uganda kuwanyanyasa raia wa Rwanda wanaotembelea au wanaoishi nchini Uganda.
![Rais Kagame ameishutumu Uganda kwa jaribio la kutaka kuangusha utawala wake](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/B3F4/production/_105986064_4bb989f9-5d72-4476-81d3-0af272a81f6d.jpg)
''Ni mgogoro ambao ukiangalia hali ilivyo bilashaka unataka ufumbuzi wa haraka'' anasema mchambuzi wa masuala ya siasa za Afrika, Khalid Hassan.
Aliongezea kusema kuwa kabla ya ziara ya rais Kenyatta nchini Rwanda rais Kagame mwenyewe alizuru Tanzania na kufanya mazungumzo y afaragha na mwenyeji wake rais John Magufuli.
Bwana Khalid, anasema huenda viongozi hao huenda walizungumzia suala la Rwanda.
![Rais wa Rwanda Paul Kagame na rais wa Tanzania Dokta john Pombe Magufuli](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/139C4/production/_105942308_1180ebfb-100a-4b07-9c48-82744137ff6e.jpg)
''Hii ni moja ya sababu hawakuwapatia wanahabari nafasi ya kuweza kufuatilia haya ili kusije kukatokea joto jingine ambalo linaweza kukwamisha juhudi ambazo zimeanzishwa''
Rwanda imeamua kutumia njia hiyo kutatua mzozo kati yake na Uganda ukifuatilia kwa makini matukio ya hivi karibuni.
Walikoanzia Kagame na Museveni:
Rais Kagame, alipokea mafunzo ya kijeshi katika mataifa tofuati ikiwemo nchini Uganda na Tanzania yaliomfanya kuonekana kama mpanga njama mzuri wa kijeshi.
Ameishi kama mkimbizi katika nchi hiyo jirani Uganda kwa miaka mingi.
Yeye alikuwa mfuasi muasisi wa jeshi la waasi la rais Yoweri Museveni mnamo 1979.
Alikiongoza kitengo cha ujasusi, na kumsaidia Museveni kuingia madarakani mnamo 1986.
Lakini muungano huu uliingia dosari wakati wa vita vya Congo kati ya mwaka 1998 na 2003 wakati mataifa hayo mawili yalipounga mkono makundi hasimu ya waasi.
Hatahivyo, kadri muda ulivyosogea, mataifa hayo yalipatana taratibu.
Rwanda imekuwa ikiishutumu Uganda kwa kuyasaidia makundi yanayopingana na serikali yake, huku nayo Uganda imekuwa ikiwatuhumu baadhi nchini Rwanda kwa ujasusi.
Tuhuma ambazo pande zote mbili zinakana kuhusika nazo.
Wachambuzi wanataja kwamba kauli hizi sio nyepesi na pengine inaashiria kazi nzito iliopo.
0 comments:
Post a Comment